SCCULT (1992) Ltd imefanya kikao cha makabidhiano ya Viongozi waliomaliza muda wao wakiongozwa na Mwenyekiti anaemaliza muda wake Dkt. Gervas Machimu na Mwenyekiti mpya Dkt. Cuthbert Msuya (2021-2024). Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro Jacqueline Senzighe akimwakilisha Mrajis wa Vyama vya Ushirika.