SALAMU ZA MWENYEKITI
Kwa niaba ya Bodi ya uongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania SCCULT (1992) Ltd, napenda kuchukua fursa hii kuwasalimu kwa upendo na kuwashukuru kwa namna mlivyokubali kuwa sehemu ya historia mpya ya SCCULT (1992) Ltd yenye kubeba maono makubwa na malengo ya kuboresha Sekta ya Ushirika wa akiba na mikopo Nchini.Shukrani za pekee ziwaendee wasimamizi wetu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) na msimamizi Mkuu Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Shirikisho la vyama vya ushirika
Tanzania (TFC), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Shirika la ukaguzi na usimamiz wa vyama vya ushirika (COASCO), Shirikisho la vyama vya ushirika wa akiba na mikopo Afrika (ACCOSCA) pamoja na vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo SACCOS wanachama na
wasio wanachama. Aidha, ninawashukuruku wadau wetu kama Saving Banks Foundation for international Cooperation (SBFIC) kwa ushirikiano wameouonesha katika katika shughuli mbalimbali za SCCULT (1992) Ltd na wanachama wake. Nipende kuwahakikishia kuwa SCCULT (1992) Ltd tumekusudia kutoa huduma bora za mafunzo na ushauri wa kitalaamu kwa SACCOS
kwa viwango stahiki ili kuwezesha SACCOS kuwa shindani, kuboresha uendeshaji wake katika soko huru la fedha. Kwa mwaka 2021, SCCULT (1992) Ltd imejipanga kuboresha Mifumo yake ya ndani, uwezo wa rasilimali watu, mahusiano na wadau wake na kuongeza mtandao wa washirika na watalaamu ndani na nje ya Nchi kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora, zinazoendana na mahitaji ya vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo lakini pia kuwezesha mabadiliko chanya na ya haraka kwa SACCOS yanatokana na mabadiliko
ya mazingira ya soko la huduma za fedha. Wito wangu kwa Wanachama, Viongozi, na watendaji wa vyama vya Ushirika wa Akiba
na Mikopo SACCOS ni kuwasihi watambue umuhimu wa elimu kuwa ndio nyezo kuu ya kuwawezesha kuongeza stadi, ujuzi na kutengeneza mahusiano ya kisekta ambayo yatasaidia kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa SACCOS. Natoa wito kwa wana SACCOS kuhakikisha tunatimiza vema msingi huu namba 5 wa ushirika unaohusu Elimu, Mafunzo na taarifa na SCCULT (1992) Ltd ni sehemu sahihi kuhakikisha tunaishi msingi huo.

DOWNLOAD HERE:MPANGO WA ELIMU NA MAFUNZO KWA MWAKA 2021